Blood Sunday

I  Midundo ya Reggae Inarindima hewani Na kuchanganyika Na macheo Katika jiji Vioo, madirisha Na milango Inasalimu amri Kutoka kumbo kali Za wenye njaa Na matarajio Ya miongo miwili. Ndani ya maduka Mawimbi ya watu Yanapaa, kushuka Na kupanda kwingineko Huku rafu na kuta Zikibadilika sura Kama tanzu za miti Kiangazi kinapojiri. Vifaa vya kila […]

Shoulder to Shoulder

Baridi kutoka mlima mwa Kenya inaingia Na upepo unavuma, misitu ya Nyandarua ukipasua Lakini mimi ni mwanamke wa Kirinyaga                 baridi sitaisikia                 chochote sitakisikia      isipokuwa sauti ya ardhi yetu                                 nchi yetu                                 polepole ikinililia. Nyumbani…                 kuponda unga kunatusubiri                 kuchuna mboga kunatusubiri                 kuchanja kuni kunatusubiri                 na watoto                                 watoto […]

Door

Ama utapita katika mlango huu au hutapita. Ukipita kuna hatari ya jinalo kulisahau. Hayo ni matata Mambo hukutizama mara mbili mbili Nawe sharuti utazame kando uwache yatendeke.                 Usitafute vita. Usipopita Huenda ukakuta maisha mema ya kufuata ukahifadhi mawazo yako ukaendelea na kazi yako ukafa kishujaa nchini mwako lakini mengi huenda yakakupita mengi yakakupofua, upofu […]

In Prison (Kizuizini)

Nikiwa na njaa na matambara mwilini           nimehudumika kama hayawani Kupigwa na kutukanwa           kimya kama kupita kwa shetani. Nafasi ya kupumzika hakuna           ya kulala hakuna           ya kuwaza hakuna. Basi kwani hili kufanyika. Ni kosa gani lilotendeka Liloniletea adhabu hii isomalizika? Ewe mwewe urukae juu mbinguni           wajua lililomo mwangu moyoni. Niambie: pale […]

The Well

Kisima cha maji ya uzima ki wazi Na vyura katika bonde la taaluma watuita Tujongee kwa mahadhi yao Yaongozayo pandikizi la mtu Kwa hatua ndefu litembealo Na sindano ya shaba kitovuni Upinde na mishale mkononi Kisha likapiga goti kisimani Tayari kumfuma akaribiaye Maana shujaa hafi miongoni mwa wezi Bali kama simba mawindoni. Hatuwezi tena kuteka […]

Literature

Maneno yangu kumeza tena sasa siwezi. Lakini kuonyesha ukweli na kuutafuta Nitaendelea: mimi ni kama boga. Nimepandwa katikati, bustanini, Na kama boga nitatambaa chini Zote pande, kuikwea miti ya hekima Na yote magugu koo kuyakaba. Bila woga, bila nyuma kurudi nitashambulia Ya binadamu matendo bado yakihema.             Halafu wakati             Ujao utafika             Matunda nitatoa […]

This Love

Ewe bibi mwenye enzi, salamu zangu pokea Mbona unanipa kazi, pendo sijalizowea Roho ina majonzi, moyo umejiinamia Fikiri utanabahi, pendo lipi ni la kweli Ulisema wewe wangu, Mpaka mwisho wa dunia Ukaapa jina la mungu, hutobadili nia Sasa kama si mwenzangu, mbona unanikimbia Fikiri utanabahi, pendo lipi ni la kweli Siku tuliyoonana, leo naikumbukia Jinsi […]

Sing for me

Uniimbie   Si wimbo  Si shairi Si utenzi Uniimbie  Hisia zako na zangu  Hisia za wanaAdamu Hisia za wavuja jasho na damu Uniimbie  Ya maisha bora Yenye ustawi na Utu Yenye mwanga bila luku Langu Dua Likiwaka jua  Ukiiandama mwezi Giza litakimbia Mende zitaparaganyika

I am thinking now!

Nawaza! mawazo ya wachache hofu ya wengi kijiweni wanapayuka ujasiri umeyeyuka matumaini yamesinzia ndoto zimetoweka matamanio yametoroka  

Euphrase Kezilahabi

Euphrase Kezilahabi, Tanzanian poet, novelist, and scholar, is perhaps the most widely known and acknowledged contemporary Swahili author. He was one of the first African writers to publish a collection of free verse poetry in Swahili, and he has had a great impact on the development of the genre of the novel in Swahili. Kezilahabi […]