Sing for me
Uniimbie Si wimbo Si shairi Si utenzi Uniimbie Hisia zako na zangu Hisia za wanaAdamu Hisia za wavuja jasho na damu Uniimbie Ya maisha bora Yenye ustawi na Utu Yenye mwanga bila luku Langu Dua Likiwaka jua Ukiiandama mwezi Giza litakimbia Mende zitaparaganyika